Monday, 23 April 2012

BEATRICE WILLIAM: Nimeokoka, sasa najipanga kuimba nyimbo za Dini!!!!





MSANII aliyekuwa anakuja kwa kasi katika muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva Beautrice William ameamua kuachana na nyimbo za kizazi kipya  na kujikita katika nyimbo za dini.

Beautrice ameamua kuachana na nyimbo hizo za kizazi kipya mara baada ya kuokoka na kuanza kumtumikia mungu mwezi mmoja uliopita.

Akizungumza na chanzo chetu cha habari, Beautrice alisema sasa akiri yake yote anailekeza kumwomba mungu huku akijipanga kuanza kuimba nyimbo za Dini.

Alisema aiku moja alipoamka asubuhi alitaka kutoka lakini roho yake ilikuwa ikikataa na kumtaka kwenda kanisani kuokoka.

“Siku hiyo bwana roho yangu ilikataa kabisa kutoka ikiniladhimu kwenda kanisani na nikatafuta namba ya mchungaji nikampigia nikajieleza akaniambia niende nikaenda nikaokoka”alisema na kuongeza kuwa.

“Nilipotoka kuonana na mchungaji nikaenda saluni nikanyoa nywele nikanunua magauni wakati zamani sikuwa na gauni wala sketi hata moja,nilivyokuwa navaa suruali na kaptula nilikuwa najiona hakuna mtu wa kunizengua awe mwanaume wala mwanamke lakini kwa sasa nimemrudia mungu najiona niko fiti sana na nina amani kwani hata mama yangu hakuamini”alisema.

Aliongeza kuwa miaka ya nyuma alikuwa akipata ushahuri kutoka kwa watu mbalimbali wakimtaka kuachana na kuvaa mavazi hayo na kuvaa mavazi ya kike alikuwa akiwaona kama hawamtakii mema na kusema kuwa kwa sasa anayakumbuka maneno yao.

                                      HABARI NA SAYARI

1 comment:

  1. Kila la kheri binti kwa safari ya maisha yako,Mungu atosha!

    ReplyDelete