NA NASRA ABDALLAH
WAKATI kukiwepo na taarifa kuwa, marehemu Steven Kanumba alitabiri kifo chake kupitia filamu yake ya ‘Power and Love’ iliyokuwa katika hatua za uhariri, aliyeigiza naye kama mke wake katika filamu hiyo, Irene Paul, amesema maneno hayo hayana ukweli wowote.
Irene alisema kutokana na uzushi huo, alilazimika kumpigia simu anayeeneza taarifa hizo na kumueleza kwamba, amuache marehemu apumzike kwa amani na kuepuka kutumia jina lake kupata umaarufu.
“Jamani mimi ndiye niliyecheza kipande cha mpenzi wa Kanumba ambaye nilimsaliti baada ya kunipatia figo yake moja.
“Filamu hiyo inaelezea namna Kanumba alivyoweza kunipatia figo hiyo baada ya mimi kupata tatizo la figo, na alikuwa akifanya hivyo kwa kuwa alinipenda sana kwa mazingira ya kimchezo.
“Lakini, wakati huohuo mimi nilikuwa na mpenzi wangu mwingine tajiri (Patcho Mwamba), aliyenikimbia baada ya kuona nimepatwa na matatizo.
“Mwisho wa siku ninapona, na nagundua kuwa nahitaji msaada mwingine wa kulipiwa kodi ambapo ninapomwarifu Kanumba, yeye ananijibu kuwa hana fedha kwa wakati ule kwa kuwa naye alikuwa katoka kulipia kodi ya nyumba anamoishi, pia hakuwa na uwezo,” alisema Irine na kuongeza:
“Majibu hayo yananifanya nirudiane na mpenzi wangu wa awali huku nikimpa maneno ya kejeli Kanumba kuwa siwezi kuwa na mwanaume suruali na pale anaponishika ili kunielewesha mapenzi yake juu yangu, namsukuma na kudondokea kwenye kiti kisha mimi naondoka zangu na kumuacha pale.
“Sehemu hiyo ndio inatafsiriwa vibaya na huyo mtoa habari eti alidondoka chini na kupoteza maisha ambapo daktari aliyethibitisha kupoteza maisha, ndio huyo aliyefanya hivyo siku ya kufa kwake Muhimbili… Hapana tusikitumie vibaya kifo cha Kanumba,” aliasa Irene na kusisitiza:
“Napenda kuwahakikishia Watanzania hakuna kitu kama hicho, ukweli wa hili ninaloliongea watakuja kuliona pindi filamu itakapotoka labda tu waamue kubadilisha kwa makusudi kipande hicho na si vinginevyo,” alisema.

Irene alisema kitu ambacho kinamumuuma zaidi katika kifo cha Kanumba, ni pale Kanumba alipomuita wakati anaigiza kipande alichokuwa akimlalamikia mama yake kwanini binadamu wamekuwa wepesi kusahau mema anayowafanyia kwa kuwa alimpenda sana mwanae na ndiyo maana aliamua kumtolea figo yake moja na kumuahidi alikuwa tayari kumpa roho yake kama ingetakiwa kuonesha upendo wake juu yake.
Alisema, wakati anaigiza kipande hicho ambacho hata hivyo kinaelezwa Kanumba aliamua kukiingiza ghafla kwa kuwa hakikuwepo kwenye script tangu awali, Irene alisema alimuita peke yake amuangalie jambo ambalo lilimtoa machozi baada ya kumwona akiigiza.
Alisema mpaka sasa anajiuliza ni kwa nini Kanumba aliamua kumuita wakati hakuwa akihusika katika kipande hicho kwani mara nyingi katika filamu kama mtu hahusiki, hapaswi kuwepo kwenye eneo husika.

CHANZO CHA HABARI HIZI KUTOKA GAZETI LA SAYARI
No comments:
Post a Comment