Taarifa rasmi ya kanisa hilo imesema kuwa sheria hiyo iliyopendekezwa imeleta mgawanyiko na ni yenye mapungufu -na inayotishia kuleta Uhasama mkubwa baina ya Kanisa na Serikali.
Ikitoa jibu lake kuhusiana na swala hilo nchini Uingereza na Wales, kanisa imesema kuwa sheria hiyo haina uzito.
Mpango wa serikali kutaka kuruhusu ndoa za jinsia moja ifikapo mwaka 2015, huenda ikahujumu maadili ya kanisa la kitaifa. Hii ndio ilikuwa kauli ya kanisa.
Hata hivyo, taarifa kutoka wizara ya mambo ya ndani zimesema kuwa makanisa hayatashurutishwa kufungisha ndoa za jinsia moja na kwamba serikali itazingatia maoni kutoka pembe zote kabla ya kutunga sheria.
Nayo mashirika ya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wametuhumu kanisa kwa kusambaza uvumi.
Kanisa linasema kuwa hatua yoyote ya kuruhusu ndoa kuwa kati ya wapenzi wa jinsia moja inakiuka maadili ya kanisa ambayo yamekuwa msingi wa kanisa kwa karne nyingi na ambao unasisitiza kuwa ndoa ni kati ya mke na mume wala sio vinginevyo. Aidha inasema kuwa kufanya hivyo itakuwa ni kuhujumu maana hii ya ndoa.
ENDELEA KUSOMA HAPA:http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2012/06/120612_gay_sheria.shtml
No comments:
Post a Comment