Tuesday 26 June 2012

URAIS NI WITO: MEMBE


Akizungumzia juu ya habari ambazo zimevuma hapa nchini juu ya kuitabiria ushindi Chadema 2015, Membe alisema hakuzungumza juu ya swala hilo, hivyo anaomba redio zitafute mkanda uliorekodi maongezi yake na vijana wa chadema"Redio tafuteni mkanda, Clouds mnisaidie kuutafuta huo mkanda uliorekodiwa maongezi kati yangu na vijana wa Chadema na kama kutakuwa na maneno niliyozungumza kuitabiria chadema nitawajibika," alisema Membe.

  • Kwenye kipindi cha Breakfast leo, pale alipotakiwa kuelezea juu ya uvumi unaovuma kuwa anatarajia kugombea urais 2015.
  • Membe alisema urais ni wito, na siyo urais tu hata uongozi wowote ule, watu 2015 wataangalia umefanya nini jimboni kwako na siyo kuoneka unaongea sana kule Bungen halafu jimboni kwako hakuna kitu. Cha msingi ni wananchi wako wakuone umewafanyia nini.
    Muendelee kusali sana nami nasali nikioteshwa 2015 nitakuja hapa tena kuzungumzia swala hili la kugombea urais. "Kuna wahariri wa habari wanne (bila kuwataja majina) kwani walinipigia simu wakitaka niwafafanulie, kwani walisema walitumiwa habari hiyo na wakasisitizwa waitoe lakini hawakufanya hivyo walibalance kwanza, huo ndo ukomavu tunaotaka," alisema Membe.

    Hayo yamezungumzwa na waziri wa mahusiano ya kimataifa, mheshimiwa Ben Membe alipokuwa akihojiwa na mtangazaji wa clouds fm, Gerald Hando,



    MAENDELEO MIKOA YA KUSINI MWA TANZANIA
    Akizungumzia swala la maendeleo mikoa ya kusini mwa Tanzania, Muheshiwa Membe alisema maendeleo yakua kwa haraka sana kwenye mikoa hiyo kutokana na Gesi nyingi iliyogunduliwa huko. 


No comments:

Post a Comment