Friday, 20 July 2012

MENEJA WA MELI ILOYOZAMA ZANZIBAR AKAMATWA,VIFO VYA FIKIWA WATU 63, SERIKALI YATANGAZA SIKU TATU MAOMBOLEZO

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Omari Hassan Mnkhon ambaye ni Meneja wa boti ya Mv Skagit, kwa ajili ya mahojiano baada ya kubainika kwamba kumekuwa na kasoro za kumbukumbu katika taarifa za hiyo.Wakati Jeshi hilo likimshikilia meneja huyo, hadi jana jioni saa 10:30, vikosi vya uokoaji vilifanikiwa kupata maiti 63, huku 29 kati yao ikiwa imetambuliwa majina namba za tiketi na sehemu wanakotoka marehemu.  

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa meneja wa boti Mkoa wa Dar es Salaam, anashikiliwa ili kuweza kusaidia jeshi la polisi kupata taarifa za kina kuhusu za meli hiyo.

Kova alisema tukio hilo linagusa maeneo mengi ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam ambako safari za meli hiyo huanzia na kuongeza kwamba, wanamshikilia meneje huyo baada ya kukosekana taarifa muhimu juu ya safari za boti hiyo.

“Tunamshikilia meneja wa meneja hiyo ili atusaidie kutupa taarifa za kina, kwani tukio hilo sio dogo na uchunguzi wa kina unatakiwa kufanywa,” alisema Kova na kuongeza;

“Jeshi la polisi litafanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo na mamlaka zinazohusika, ili kujua chanzo cha ajali pamoja na kupata taarifa za kina za boti hiyo tangu ilipoanza safari yake,” alisema.


Maiti zilizotambuliwa

Hadi saa 10 jioni jana, maiti 63 zilikuwa zimepatikana na watu 145 kuokolewa wakiwa hai. Hata hivyo kati ya maiti hizo zBaadhi ya maiti waliotambuliwa pamoja na umri wao na maeneo wanayoishi katika mabano ni Anita Emanuel (42,  Kibamba -Dar es Salaam), Rukiya Issa Muombwa (miezi 2, Meli nne –Fuoni Zanzibar ), Halima Ali Khamis (23, Mtopepo- Zanzibar), Kolin Krispin (miezi 9, Kunduchi - Dares Salaam) na Rahma Ali Abdalla (miaka 52, Mfenesini - Zanzibar).

Maiti wengine ni  Said Jumanne Masanja (miaka 9, Nzega Tabora), Sauda Abdalla Omar (22, Ole Pemba), Said Juma Said (36, Arusha),  Amina Abdalla Tindwa, (miezi 6, Fuoni), Halima Ramadhani Kilimo, (53, Morogoro), Khadija Omar Ali (58), Amina Hamir Bakari (39, Chukwani - Zanzibar), Mwanahamisi Mshauri (42, Kibandamaiti),  Ali Hamdu Othman (35, Mkwajuni) na Mohamed Said Salum (40, Magomeni Mikumi - Dares Salaam).

Wengine ni Amina Ahmed Ramadhani (21, Michenzani zanzibar ), Mgeni Juma Halfani (25, Daraja Bovu), Khadija Rajab Kibune (22, Fuoni), Maua Ramadhani Feruzi (29, Mwembeladu), Hussein Ali Khamis (4, Mwanakwerekwe) na Sabiha Heri Mbarouk (25, Mgeleme, Chakechake-Pemba).

Pia wamo Halima Ali Mohamed (35, Kiwengwa- Zanzibar), Asia Juma Khamis (29, Kiembe Samaki), Yusuf Hasan Yusuf (7, Chamanzi, Dar es Salaam), Batuli Abrahmani Amir (20, Jang'ombe), Fatma Said Sultani (54, Msasani Dar es Salaam), Juma Jafari Shajak (Miezi 6, Kimaneta - Tanga) na Mohamed Ali Ngombe (41, Buguruni - Dares Salaam).

Serikali yatangaza siku
tatu za maombolezo 

Kufuatia msiba huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Julai 19 hadi Julai 21 mwaka huu. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein alisema bendera zote zitapepea nusu mlingoti na shughuli zote zinazoambatana na sherehe na burudani zimefutwa kwa muda huo lakini kazi na shughuli za Serikali zitaendelea kama kawaida

Nayo Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi ilitangaza siku tatu za maombolezo kufuatia msiba huo mkubwa uliolikumba taifa.
 
Lukuvi aliwaambia waandishi katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zitapepea nusu mlingoti na shughuli za starehe zitasimamishwa ila kazi zitaendelea kama kawaida. 
ilizopatikana, matiti 34 zilichukuliwa na ndugu zao. 
Rais Shein amewahakikishia wananchi na hasa waliopoteza jamaa zao kuwa Serikali itabeba gharama zote za mazishi na huduma za matibabu kwa majeruhi.
 ENDELEA KUSOMA HAPA:http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/24888-meneja-meli-iliyozama-zanzibar-akamatwa.htm

No comments:

Post a Comment