Friday, 5 October 2012

WAZAZI WA LINAH WAKERWA NA VIVAZI VYAKE VYA KIMITEGO!

MWANAMUZIKI Estelina Sanga ‘Linah’ amefunguka kuwa, wazazi wake wanakerwa sana na tabia yake ya kuvaa nusu utupu.
Akipiga stori na mtandao mmoja wa habari za kijamii na mastaa Bongo, Linah alisema mara kwa mara wazazi wake wamekuwa wakifurahishwa na kazi yake ya muziki anayofanya lakini hilo la mavazi wamekuwa wakilikemea sana.
“Nimewazawadia wazazi wangu nyumba ya shilingi milioni 30 lakini licha ya kujua kuwa hayo ni matunda ya kazi ya muziki ninayofanya, mpaka sasa hawakubaliani na mavazi ninayovaa kwenye shoo.
“Nimejitahidi sana kuwaelezea wazazi wangu wanielewe kuwa litakapotokea tatizo lolote itakuwa ni bahati mbaya tu lakini siyo kwa makusudi. Nyimbo zangu baba anazisikiliza na anazipenda na anakubali ninaimba kitu ambacho kipo, ila ubishi mkubwa kati yangu na yeye ni mavazi,” alisema Linah.
chanzo:http://www.globalpublishers.info

No comments:

Post a Comment