Friday 2 November 2012

CHUPUCHUPU GARI LA WOLPER KUUNGA LOTE BAADA YA KUCHOMWA MOTO!!!



GARI aina ya Toyota Brevs la staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper limechomwa moto nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar.
Kwa mujibu wa staa huyo, tukio hilo limetokea hivi karibuni wakati alipokuwa safarini Morogoro kwa shughuli zake za kisanii.
“Mi sikuwepo nyumbani, ila kuna mtu alifika na kuwasha moto kwenye matambaa baada ya kuyapaka mafuta ya taa au petroli na kurusha juu ya tenki la gari,” alisema Wolper.
  Staa huyo alisema kuwa, tenki lilianza kuungua na baadaye moto ukashuka hadi kwenye gari na kuanza kuliunguza.
“Bahati nzuri mlinzi aliyekuwa upande wa pili aliwahi na kuuzima moto ule kabla gari halijaungua sana.” 
Alipotakiwa kuwataja watu anaowahisi kumtendea unyama huo, Wolper alisema kuwa anawahisi watu wawili ambao hata hivyo alikataa kuwataja majina yao.
Chanzo:globalpublishers

No comments:

Post a Comment