Wednesday, 12 December 2012

Polisi Ilala wamsaka aliyetupa kichanga


POLISI wilayani Ilala wanamtafuta mwanamke aliyetupa mtoto wake mchanga kwenye eneo la Machimbo na kuokotwa akiwa amefariki.
Kichanga hicho cha jinsi ya kike, kinakadiriwa kuwa na umri wa siku mbili, kimekutwa katika machimbo ya mchanga maeneo ya Majohe, Gongo la Mboto.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieth Mnagi ilisema kuwa kiliokotwa Jumapili jioni eneo la Mojohe Machimbo.
Alisema maiti ya kichanga hicho ilikutwa  ikiwa imeviringishwa kwenye khanga na kuwekwa kwenye eneo wazi.
Alisema  uchunguzi wa awali umebaini kuwa juu ya khanga hiyo kulikuwa na lebo iliyoandikwa Julieth Godwin ,F.Kiice  na terehe ya Desemba 7 yenye kutambaulisha lebo ya hospitali na jina la mama mzazi wa mtoto.
Alisema juhudu za kumtafuta aliyefanya kitendo hicho zinaendelea na mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana.
Wakati huohuo Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri katia ya miaka 25-30 amekutwa amefariki dunia baada ya kutapika damu nyingi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema tukio hilo lilitokea Desemba 9 saa 4:00 usiku maeneo ya Mbagala Mzarambauni.
Alisema chanzo cha kifo chake hakijatambulika  na mwili umehifadhiwa katika Hospital ya Temeke kwa uchunguzi.
Aliwataka  ndugu na jamaa ambao wamepotelewa na mtu wa aina hiyo kufika polisi ili kupata taarifa zaidi. Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi wa matukio hayo.
chanzo:mwananchi

No comments:

Post a Comment