Tuesday, 23 April 2013

Lady Jaydee afunguka ya moyoni


MSANII mahiri anayeendelea kutesa katika anga la muziki, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ wakati akitarajiwa kuachia albamu yake ya sita, ameelezea yale yaliyo moyoni mwake.
Albamu hiyo aliyoipa jina la ‘Nothing But The Truth’ ameelezea kile ambacho kimejificha katika moyo wake.
Akizungumzia ujio wa albamu hiyo, ambayo itaingia sokoni Mei 31, mwaka huu, ikiwa imewashirikisha wasanii kama Prof. Jay, Yahya, Njiwa na bendi yake ya Machozi, alisema kuwa anaamini itawabamba mashabiki kutokana na namna alivyoeleza yale anayojisikia kutoka moyoni mwake.
Albamu hiyo ina nyimbo saba, ambazo ni ‘Joto Hasira’, ‘Historia’, ‘When You Cry’, ‘Msichoke’, ‘Tell Him’, ‘Nimekusamehe’ na uliobeba albamu, ‘Nothing But The Truth’.
Albamu za msanii huyo ni pamoja na ‘Machozi’ aliyoitoa mwaka 2000, ‘Binti’, ‘Moto’, ‘Shukrani’ na ‘The Best of Lady Jaydee’ iliyotoka mwaka 2012.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment