Monday, 15 April 2013

Maiti ya kichanga yakutwa mtoni


MTOTO mchanga wa siku moja amefariki dunia baada ya mama asiyefahamika kumtupa katika mto eneo la Sinza kwa Remmy, jijini Dar es Salaam.
Kichanga hicho kiligunduliwa juzi na wananchi walikuwa wakiendelea na shughuli zao katika maeneo hayo.
Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela ilieleza kuwa mwili wa kichanga hicho cha kiume umehifadhiwa katika hospitali ya Mwanayamala na polisi wanaendelea kumsaka mwanamke aliyefanya kitendo hicho.
Wakati huohuo, mwendesha pikipiki, Hussein Mkana (34) Mkazi wa Pugu amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Fuso.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa moja jioni, maeneo ya Mwisho wa Barabara ya Lami Baghdad wakati hilo gari likitokea Pugu kuelekea Gongo la Mboto.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Amana na polisi wanamsaka dereva na Fuso.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment