MBUNGE wa Viti Maalumu, Susan Kiwanga (CHADEMA) na maofisa wa Benki ya NMB
Tawi la Kilombero, wamejikuta wakidondosha machozi baada ya kushuhudia wanafunzi
wakiwa wamekaa kwenye tope huku wakiendelea na masomo.
Tukio hilo lilitokea juzi katika shule za msingi Ntyangimbole na Kidete, zilizopo wilayani hapa wakati viongozi hao walipopeleka msaada wa madawati.
Pia viongozi hao walilazimika kuchangishana fedha papo hapo kwa ajili ya kununua mbao mbili za kuandikia walimu darasani.
Uamuzi huo ulifikiwa baada ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ntyangimbole, Emmanuel Njavike, kusema kuwa mbali na watoto kukaa kwenye tope, hakuna vifaa vya kufundishia kama mbao za kuandikia, meza na vitabu, hivyo kuwalazimu walimu kufundisha kwa uzoefu.
Katika risala ya Shule ya Msingi Nyangimbole iliyosomwa na Mwalimu Asunta Mbuja, mbele ya ujumbe huo uliotoa madawati 38 kwa kila shule, walimu hao walisema ukosefu wa madarasa imara umetokana na serikali kutelekeza nguvu kazi za wananchi waliojitokeza kujenga vyumba viwili vya madarasa.
Wakijibu madai hayo kwa nyakati tofauti, Mbunge Susan aliahidi kufikisha kilio hicho bungeni kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kulishawishi baraza la madiwani katika halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa upendeleo maalumu kuziwezesha shule za pembezoni kuwa na majengo imara ili wanafunzi wapate elimu bora.
chanzo:daima

No comments:
Post a Comment