Tuesday 4 June 2013

Shoo za Jide, Mwana FA sasa Juni 14


SHOO zilizokuwa zifanyike Mei 31, mwaka huu katika kumbi tofauti kati ya Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Judith Wambura, Lady Jaydee’ au Jide, sasa zinatarajiwa kufanyia Juni 14.
Wasanii hao waliamua kuahirisha shoo zao kutokana na msiba wa Albert Mangwea ‘Ngwair’ uliotokea Mei 28 nchini Afrika Kusini.
Mwana FA alikuwa wa kwanza kueleza siku ya kufanyika kwa shoo yake, ambapo alisema kuwa, kama mazishi ya Ngwair yatafanyika mapema, anatarajia Juni 14 kufanya shoo hiyo.
“Sina uhakika, lakini naitaja Juni 14 kama siku yangu ya kufanya shoo niliyoiahirisha kama ‘brother’ tutakuwa tumeshampumzisha,” alisema.
Kwa upande wa Lady Jaydee, alisema: “Juni 13, ni siku ya mahakamani, Juni 14 mwaka huu ni miaka 13 ya Jide na Juni 15 ni siku ya kuzaliwa kwangu, ni Juni mwezi wangu,” alisema.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment