Monday 12 August 2013

Ana mimba ya nje, lakini anakunywa sumu kisa mume kaoa mke mwingine!

 “Huyu mama ana mahusiano na mwanaume mwingine wa nje na inasadikika ndiye aliyempa ujauzito alio nao hivi sasa.
“Siku aliposikia mumewe kaoa mke mwingine, (kama dini inavyoruhusu), huyu mama alitaharuki na kwenda dukani kununua sumu ya panya na kuinywa hali akiwa na ujauzito.
Mimi ndipo nikashangaa ana maana kuwa anampenda sana mumewe? Au vipi! Mbona ana ujauzito wa mtu mwingine? Sijajua huyu mama ana mapenzi ya aina gani.
“Taarifa zaidi ni kwamba mama huyo aliyekunywa sumu alinusurika kifo kwa jitihada za majirani waliomkimbiza hospitali Mwanamama aliyebugia sumu ya panya akijaribu kujiua alifanya hivyo wakati akiwa na mimba ya mwanaume wa nje ya ndoa.
Bahati yake aliokolewa na majirani waliomkimbiza hospitali na kuepuka kifo. Habari za baadaye zinasema kuwa mama huyo tayari alishajifungua mtoto ambaye sasa na umri wa mwaka na nusu.
Inaelezwa pia kuwa yule mwanaume wa nje tayari alishatuma wadadisi na kumpiga picha mtoto yule na kisha kwenda kuwaonyesha ndugu zake. Mtoto huyo anafanana kabisa na mwanaume huyo wa nje na siyo mume huyu wa ndoa.
Hata hivyo, dini inambana yule mwanaume wa nje kumdai mtoto huyo endapo itathibitika kuwa ni wake kutokana na msemo uliozoeleka kuwa kitanda hakizai haramu.

Na baba huyu mwenye mke aliyetaka kujiua, bado hajagundua kuwa mtoto huyo siyo wake kwani anaamini yule ni mkewe na wala hajamuacha na kwamba yule mwingine aliyemuoa pia ni mkewe wa pili kwani dini inamruhusu.
Naam. Hofu ya msomaji wetu aliyetudokeza kisa hiki ni je, mapambano dhidi ya gonjwa hatari la ukimwi yatafanikiwa? Hata kama ni wivu kwa mumewe kuoa mke mwingine, mbona yeye amevunja uaminifu na kujihusisha kimapenzi na mwanaume mwingine?
Mpenzi msomaji, hapa ni dhahiri kwamba mke huyu aliyetaka kujiua hana uvumilivu, hana uaminifu, ana wivu wa kijinga huku akijua kuwa mumewe dini inamruhusu kuoa mwanamke zaidi ya mmoja.
Kama kweli alilijua hilo, kwanini yeye(mama) aamue naye kuwa na mume zaidi ya mmoja nje ya ndoa wakati kwa upande wa wanawake hairuhusiwi? Kama alitaka mwanaume mwingine, ilitakiwa aombe talaka, akubaliwe, kisha akajiegemeze kwa huyo mwanaume mwingine wa nje. Au siyo?
Hili ni tatizo kubwa sana katika familia zetu nyingi. Mwanamke kutaka kushindana na mumewe kwa kila jambo alifanyalo. Ni vyema kinamama wakatambua kuwa siyo kila jambo linahitaji kufanyiwa ulinganifu/ ushindani. Mengine ni asili na yanapaswa kuheshimiwa.
Ni muhimu ikaeleweka pia kuwa mwanaume kuacha na kuona mwingine ni rahisi sana kuliko mwanamke kuachwa na kuolewa tena. Mwanamke anayejulikana kuwa akishaolewa kisha akaachika, wengi thamani yao hushuka ikilinganishwa na mwanaume aliyeacha na kuoa tena.
Tena kwa wanaume wanaweza kuonekana vidume vya mbegu pale anapoacha na kuoa mwingine na hasa iwe ni mtu mwenye uwezo mkubwa kimaisha. Anaweza kubadili wanawake vile apendavyo na wala asichujuke. Lakini mwanamke hushuka thamani kwa kiwango fulani.
Na wengi ambao utawaona wanajitutumua kama nao wana uwezo, hudiriki hata kuwarubuni wanaume ili kusogeza mahusiano karibu. Hawa ni wale wanaowakirimu wanaume ili nao waonekane mbele ya jamii kuwa wanapendwa kumbe wao ndiyo wanaolazimisha kupenda kujijengea umaarufu.
Hebu turejee kidogo kisa cha hapo juu, mwanamama aliyetaka kujiua kwa sumu anaye mumewe ndani, lakini bado anamtamani mwanaume wa nje. Inawezekana ni wivu kwamba alizoea kuwa peke yake ndani, lakini sasa mumewe amejigawa kaoa mwingine kwa hiyo penzi limegawanyika.
Anaona wakati mume akiwa kalala kwa mke mwenzie, kumbe yeye apate joto wapi? Ibilisi akamdanganya atoke nje akatafute kiburudisho. Huko nako kuna karaha zake, mahusiano yakakolea na bila kujua mimba ikanasa. Anadhani mimba ni ya mume kumbe sura itatoboa siri.
Kisa hiki kinanikumbusha ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali nchini kuhusu kinababa wengi hubambikizwa watoto. Ripoti hiyo ikasema kuwa zaidi ya asilimia 48 ya wanaume waliojitokeza kupima vipimo vya vinasaba (DNA) wamegundulika kubambikiwa watoto.
Takwimu hizo za Julai mwaka huu, ni kwa mujibu wa vipimo vya DNA vilivyochukuliwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2010.
Ripoti hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Jinai na Vinasaba, Gloria Machuve, wakati akielezea wanahabari kazi za ofisi hiyo katika uchunguzi wa vinasaba vinavyotokana na matukio na mashauri mbalimbali.
Alisema asilimia 48.32 ya watoto waliofanyiwa vipimo vya DNA kwa kipindi hicho wamegundulika hawalelewi na baba halali.
Alisema utaalamu huo wa kuchunguza vinasaba ulianza mwaka 2010, ambapo hadi kufikia mwaka 2012, wamepata mafanikio makubwa kwa kutatua mashauri na kuwatambulisha watu uhusiano wao.
Alisema kwenye utambuzi wa uhalali wa watoto, sampuli mbalimbali kutoka kwa watu tofauti walizipima na kuonyesha asilimia kubwa ya watoto hawalelewi na baba halali.
"Idadi hiyo ni kubwa watoto walioonekana hawana uhalali wa vinasaba vya mzazi wao (baba), lakini takwimu hii siyo kwa nchi nzima ila tu kwa wale wanaofika kwetu na kutatua mashauri ya kufahamu watoto wao," alisema Machive.
Alisema kwa kutumia teknolojia hiyo, sampuli za wazazi na watoto zinachukuliwa na kuingizwa katika mashine yenye uwezo wa kuchambua vinasaba na kugundua uhalali wa mtoto.
"Vinasaba huwa havidanganyi, ikiwa mtoto vinasaba vyake havifanani na baba ni dhahiri siyo wake ila alidanganywa kwa sababu mbalimbali," aliongeza.
Machuve, alifafanua kwamba vinasaba vina umbo la majimaji yenye kemikali, ambayo yana taarifa kamili ya mtu husika ikiwa ni asili yake, umbo, rangi na jinsia
chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment