Wednesday 21 August 2013

Diamond ampiga tafu dada yake

MWANADADA anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki wa bongo fleva, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’, anajipanga kuachia kazi yake mpya ambayo bado hajaipa jina hivi karibuni.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Queen Darleen, alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho ambacho ameshirikiana vema na kaka yake, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’.
Amewaomba wapenzi wa kazi zake wakae mkao wa kula kwa ajili ya kuipokea kazi hiyo kutokana na mashairi yaliyomo ndani yake kuwa na ubora na ujumbe katika jamii.
“Naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwa ajili ya kazi hii, ambayo naamini itafanya vizuri kutokana na ubora wa mashairi hayo pamoja na uwepo wa mkali huyo ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo,” alisema.
Mwanadada huyo alishawahi kutamba na kazi zake za ‘Maneno Maneno’, ‘Koi koi’, ‘Najua Wanipenda’ na nyinginezo ambazo zilifanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

No comments:

Post a Comment