Friday 16 August 2013

Mume aliyemlawiti mwanaye na kumbaka shemeji yake atishia kumuua mke.

MTANZANIA mwenye asili ya Kihindi, aitwaye Mohammed anayetuhumiwa kumlawiti mtoto wake wa kufikia na kumbaka shemeji yake hivi karibuni, ametoa vitisho vya kumuua mzazi mwenziwe kwa kutoa taarifa ya matukio hayo polisi, Ijumaa limeambiwa.
Mohammed ambaye alitoroka Kigamboni jijini Dar alikokuwa akiishi na mzazi mwenziwe huyo, pia ametishia kuichoma moto nyumba anayoishi mwanamke huyo ambaye amezaa naye mtoto mmoja.
Akizungumza na Ijumaa, mzazi mwenza wa Mohammed aliyefahamika kwa jina la Zubeida alisema baada ya mwanaume huyo kubaini analifuatilia sakata lake la kuwafanyia vibaya watoto hao, amempigia simu na kumpa vitisho kwamba ajiandae kuvamiwa usiku na kuchomewa nyumba anayoishi.
“Sina amani kabisa na hata hawa polisi siwaelewi kwa kuwa simu ya mtuhumiwa inapatikana na ananipigia kunitishia lakini wanashindwa kumkamata, nahisi kuna mchezo unaendelea kwani Mohammed ameniambia nisihangaike na polisi kwa sababu hakuna anayeweza kumkamata,” alisema mama huyo.
Mama huyo ameendelea kusema kwamba Kituo cha Polisi Kigamboni hawampi ushirikiano wa kutosha na aliamua kwenda kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Englbelt  Kiondo aliyemshauri aende kwa mpelelezi wa kesi ambaye angemwandikia barua ya kukamatwa kwa mtuhumiwa.
“Jambo hilo nimeliona kuwa ni gumu sana kwangu, nahitaji msaada na naomba Watanzania wanisaidie kwani sina amani kiukweli,” alisema.
Aidha, mama huyo ameziomba taasisi zinazoshughulikia masuala ya haki za binadamu na watoto zimsaidie katika suala hilo kwani hana njia nyingine ya kuweza kupata msaada.
Kama vile haitoshi, mama huyo ameomba msaada wa kutibiwa kwa watoto wake kwa kuwa wameathirika kwa kiasi kikubwa.
Kwa mara ya kwanza habari hii ilitoka kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi wiki iliyopita na kurushwa hewani na Redio Wapo katika kipindi chake cha Patapata.
Mohammed anadaiwa kumlawiti mtoto wa kiume wa mama huyo mwenye umri wa miaka sita aliyekuwa akilala naye chumba kimoja baada ya mkewe kujifungua.
Aidha, mdogo wa mkewe alipofika nyumbani hapo, inadaiwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiamka usiku na kujidai kwenda kuvuta sigara kumbe alikuwa akienda kumbaka.
chanzo:globalpublishers

No comments:

Post a Comment