Tuesday, 3 September 2013

Dimpoz afichua siri kolabo na J. Martin

MKALI wa bongo fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amefichua siri nzito iliyokuwa imejificha nyuma ya pazia kuwa mwanamuziki Ambwene Yessaya ‘AY’ ndiye aliyemfanikisha kufanya kolabo ya wimbo na staa wa kimataifa J.Martin.
Dimpoz ambaye ni miongoni mwa wanamuziki chipukizi wa muziki wanaokimbiza kwa sasa aliishangaza tasnia ya kizazi kipya ghafla alipojitokeza na kueleza amepata shavu la kufanya wimbo na Mnigeria J. Martin ambaye anatikisa bara la Afrika kwa nyimbo mbalimbali.

Dimpoz kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Tupogo’ alichoimba na J.Martin na alishawahi kutamba na kazi nyingine kama ‘Nai nai’, ‘Baadae’ na ‘Me and You’ ambavyo vilimtambulisha vema na kufanya vizuri katika soko la muziki huo.
Alieleza mafanikio aliyonayo katika muziki huo ni juhudi zake binafsi lakini katika anga ya kimataifa hatoweza kumsahau AY kwa kuwa ndiye aliyeweza kumkutanisha na J. Martin na kumpigia chapuo afanye naye kazi kitu ambacho kimempandisha chati katika ramani ya Afrika kuwa miongoni mwa wanamuziki walioweza kutoka.
“Ndoto zangu zilikuwa ni kufanya kazi na wasanii wa makundi makubwa duniani kama P Square lakini karata yangu ikaanza kwa kuangukia kwa J. Martin, nikiamini ni mwanzo wa safari yangu kuelekea kwenye mafaniko zaidi ya niliyonayo sasa,” alisema
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment