Friday, 13 September 2013

LULU APATA VITISHO

KUFANIKIWA kwa uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ya msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, kumemfanya kinda huyo anayetingisha katika tasnia hiyo kupata vitisho kutoka kwa mastaa wenzake.
Habari kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya fani hiyo zinasema katika uzinduzi huo, msanii huyo alifunika na kuonyesha dalili zote za kuwazima mastaa wenzake ambao kwa muda mrefu wamekuwa juu.
Taarifa hizo zinasema staa huyo wa Bongo Muvi anatafutwa kwa kila namna, usiku na mchana ili kuhakikisha nyota yake inafifia.
Madai hayo yamekuja zaidi baada ya uzinduzi huo kufana kwani pamoja na mambo mengine, hata jinsi alivyokuwa amejipanga kwa walinzi wake, lilikuwa ni jambo kubwa ambalo linafanana na inavyotokea katika shughuli za mastaa mbalimbali wa majuu.
Mwandishi wa gazeti hili aliamua kufunga safari hadi maskani kwao pande za Tegeta, lakini msanii huyo hakupenda paparazi afike kwao hivyo mazungumzo yao kufanyika kama ifuatavyo kwa njia ya simu ya kiganjani.
Mwandishi: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Salama tuu za kwako?
Mwandishi: Salama, vipi umesikia vitisho vyako kutoka kwa mastaa wa Bongo Muvi wanaodai kuwa umekuja kuwapita kisanii?
Lulu: Hapana sijasiki, lakini kama wanatoa vitisho lazima wakubaliane na ukweli kwamba lazima awepo wa kwanza na wa mwisho, wakaze buti.
Mwandishi: Umejipangaje kukabiliana na hilo?
Lulu: Najipanga kufanya kazi mimi kama mimi na wao wafanye kama wao, wakijifanya kuwa kama mimi haiwezi kuwa hivyo, mbona mastaa wa ughaibuni kama Beyonce na Rihanna wako tofauti? Lazima awepo wa kwanza mpaka wa 10 hatuwezi kulingana.
Mwandishi: Kuna lolote la kuongeza juu ya hilo ama wito kwa wasanii?
Lulu: Wajipange kufanya kazi kwa nguvu zote, wasifanye kama mimi wafanye kama wao,
Mwandishi: Asante Lulu nakutakia siku njema
Lulu: Ok, sawa kazi njema
chanzo:.globalpublishers

No comments:

Post a Comment