Tuesday, 1 October 2013

Ray C’, kuibuka na ngoma inayoitwa ‘Roho Imekuchagua Wewe Pekee’,

BAADA ya kimya cha muda mrefu, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, anatarajiwa kuibuka na ngoma yake inayokwenda kwa jina la ‘Roho Imekuchagua Wewe Pekee’, ambao upo katika hatua za mwisho za maandalizi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Ray C ambaye ameanza kujipanga kurejea upya, aliwataka mashabiki wajiandae kuendelea kupata nyimbo zake ambazo kwa asilimia kubwa zinazungumzia mapenzi.
Alisema tayari wimbo huo umefikia kwenye hatua za mwisho, hivyo muda wowote utaanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio.
“Mashabiki watanielewa, nyimbo zangu ni mwendelezo wa mambo yanayohusu mapenzi, hivi ni vitu muhimu kwa binadamu,” alisema Ray C.
Msanii huyo alisema kuwa atajitahidi kufanya nyimbo nyingine kwa haraka ili aweze kuachia albamu yake ya kwanza tangu kurudi katika ‘game’.

No comments:

Post a Comment