Ndugu aliyejitambulisha kwa jina la Rehema Issa, alisema marehemu Hamida alikumbwa na ukatili huo Jumapili iliyopita nyumbani kwake Kibondemaji Mbagala jijini Dar, lakini mwili wake ukagundulika Jumanne kufuatia harufu kali iliyokuwa ikitoka ndani ya chumba chake.
Rehema alisema ndugu yake alifunga ndoa na Yahya miaka mitatu iliyopita lakini ndoa hiyo ilikuwa ikikumbwa na migogoro ya mara kwa mara.
“Ugomvi mkubwa ulikuwa ni kuhusu ulevi wa mwanaume jambo ambalo lilikuwa likimkera sana mkewe,” alisema Rehema.
Ndugu huyo alisema kila alipokuwa anarudi nyumbani amelewa, mwanaume huyo alikuwa akimshushia kipigo mkewe na kumfanya marehemu kupeleka malalamiko yake akachukue vyombo vyake na alisema mdogo mtu huyo aliyejitambulisha kuwa ni upande wa mwanaume lakini hakukuwa na suluhu yoyote.

Habari zinadai kuwa siku moja Hamida akiwa kwao, Tabata, mume alitishia kujiua na kumfanya marehemu kwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Tabata na kufunguliwa kumbukumbu ya jalada nambaRB TBT/ RB/ 1583/ 2013 TAARIFA.
Pia Hamida alikwenda kutoa taarifa kwenye Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) ili aweze kupewa talaka yake.
Pia Hamida alikwenda kutoa taarifa kwenye Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) ili aweze kupewa talaka yake.
“Mumewe aliandikiwa barua ya wito na Bakwata lakini hakwenda.
“Siku moja mwanaume huyo alimpigia simu mkewe na kumwambia anataka kuhamia Sinza kwa hiyo aende nyumbani kwao
vingine wagawane. “Mama yetu (Zaria Munge)alimzuia Hamida kuvifuata vitu hivyo lakini marehemu alilazimisha kwa madai kuwa mumewe akihamia sehemu nyingine itakuwa vigumu kuvipata vyombo vyake,” alisema Rehema.

Inadaiwa kwamba mwanaume huyo alikwenda nyumbani kwa wakwe zake ili akamchukue mkewe wakagawane hivyo vyombo. Kutokana na shaka, marehemu aliamua kumchukua mdo go wake ili wawe wawili.
Habari zinadai Hamida na mumewe walitembea sanjari huku mdogo mtu huyo akitangulia na kwenda kufikia kwa jirani wakati akiwasubiri.
Wawili hao walipofika, mdogo mtu huyo aliwafuata kwa lengo la kuungana nao katika zoezi la kukusanya vyombo lakini sh- emeji yake alikataa na kumtaka abaki nje kisha akafunga mlango kwa ndani.
“Nilipoona shemeji amekataa nisiingie na akafunga mlango niliamua kurudi kwa yule jirani. Mara shemeji akanipigia simu kwa namba ya dada ikisema nirudi nyumbani kwani wao bado wana shughuli maalum,”
baye jina halikupatikana mara moja.
baye jina halikupatikana mara moja.
Akiwa njiani, alipigiwa tena simu na shemeji yake huyo akimwambia kuwa muda si mrefu simu zote zitazima chaji lakini asiwe na wasiwasi wowote.
Habari zinasema kuanzia wakati huo hadi saa sita usiku Hamida hakuwa amerudi kwa mama yake, lakini mara Yahya alimpigia simu mdogo huyo wa marehemu akimuulizia kama dada yake ameshafika nyum bani hapo!
“Nikashangaa sana, inakuwaje shemeji aniulize hivyo wakati niliwaacha pamoja baada ya kunizuia kuingia ndani? Kuanzia hapo nikaingiwa na wasiwasi,” alisema.
Asubuhi ya siku ya pili, ndugu wa Hamida walikwenda Mbagala na kutoa taarifa polisi ya kupotelewa na ndugu yao huyo katika mazingira ya kutatanisha, polisi walikataa kutoa ushirikiano ikiwemo kuvunja mlango wa nyumba hiyo ili kujiridhisha ndipo waliondoka huku mioyo yao ikiwa imegu bikwa na wasiwasi.
Jumanne iliyopita mama mzazi alipokea simu kutoka kwa mjumbe wa eneo la Kwamjerumani (ilipo nyumba ya Yahya) na kumtaarifu kuwa kuna harufu kali sana kutokea kwenye nyumba ya Yahya hivyo wafike mara moja kwa ajili ya ukaguzi.
“Simu hiyo ilinishtua sana, nikawataarifu ndugu akiwemo dada wa marehemu, tukaenda,” alisema mama mzazi.
Akaendelea kusema kuwa baada ya kufika mahali hapo, walichukua uamuzi wa kuvunja mlango kwa kupewa ruhusa na mjumbe ambapo chumbani waliukuta mwili wa Hamida ukiwa kitandani.
Akaendelea kusema kuwa baada ya kufika mahali hapo, walichukua uamuzi wa kuvunja mlango kwa kupewa ruhusa na mjumbe ambapo chumbani waliukuta mwili wa Hamida ukiwa kitandani.
Marehemu alikuwa ameshindiliwa nguo kinywani na kufungwa kitambaa shingoni huku mwili wake ukiwa ndani ya nailoni ikionekana kuwa unyon-gaji umefanyika.
Baada ya taratibu zote ku fanyika mwili wa marehemu ulipelekwa katika Hospitali ya Temeke kwa uchunguzi zaidi.
Marehemu Hamida alizikwa Jumatano iliyopita katika Kijiji cha Mzenga, Bagamoyo, Pwani. Ameacha mtoto wa kike aitwaye Tayana. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali panaposta- hiki. Amina.
Marehemu Hamida alizikwa Jumatano iliyopita katika Kijiji cha Mzenga, Bagamoyo, Pwani. Ameacha mtoto wa kike aitwaye Tayana. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali panaposta- hiki. Amina.
No comments:
Post a Comment