BAADA ya kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Number One Remix’ aliyoimba na msanii kutoka Nigeria, Davido, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’ amesema kwa sasa anafanya kazi nyingine na mkali wa nchi hiyo, Iyanya.
Kwa mujibu wa Diamond Platinum, safari yake ya Nigeria imempa mafanikio makubwa na kwamba, ngoma hiyo aliyofanya na Iyanya ipo tayari, anachosubiri ni kuisambaza tu.“Huwezi ukaachia kazi mfululizo kama njugu, nimetoka kusambaza kazi niliyofanya na Davido, nalisikilizia soko langu baada ya muda mfupi nitaisambaza,” alisema.
Alisema, mbali na wasanii hao, pia kwa sasa ana mpango wa kufanya kazi na msanii wa nchi hiyo, Mr, Flavor ambaye pia ni mmoja wa wakali wanaotikisa katika nchi hiyo.
“Nataka kufanya kazi na wasanii wakubwa ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki huu ili niweze kufanikiwa zaidi, kikubwa ni sapoti kutoka kwa mashabiki na vyombo vya habari, hivyo wapenzi wangu wasubiri vitu vizuri zaidi vinakuja,” alisema.
Diamond ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki huu, kutokana na uwezo wake wa kutunga mashairi ambayo yanawagusa wengi
chanzo:tz daima
No comments:
Post a Comment