Monday 28 April 2014

Nafurahia mto wa kulalia kuliko mume wangu…nisaidieni jamani!


 Nisaidieni jamani. Niliolewa na ninaishi vizuri kwenye ndoa yangu. Mume wangu alisafiri kikazi akakaa miezi sita. Nilikuwa mwaminifu kwa mume wangu hivyo hamu ya tendo la ndoa linaponijia nachukua mto wa kulalia na kuutumia 

Niliendelea hivyo kwa muda mrefu. Ghafla nikawa sina hamu na mume wangu kwani raha niliyokuwa napata nikiwa mwenyewe ilikuwa kubwa kuliko nikiwa na mume wangu. Wakati mwingine nikiwa na mume wangu inabidi nijifanye kama nimeridhika kumbe sivyo asije akagundua kuwa simfurahii.

Mpenzi msomaji haya ni matatizo makubwa katika mahusiano hasa hilo la kwanza la bibie kuweka mawazo yake kwenye mto, jambo ambalo linamtesa.


Mimi nilijaribu kumsaidia kwa kumshauri mambo mawili; Kwanza nilimpa namba ya simu ya daktari ambaye atazungumza naye  amweleze tatizo hilo ili aweze kumshauri njia ya kuondokana nalo.

Pili nilimshauri azame kwenye maombi ya kiroho kwani katika hali ya upweke shetani huchukua nafasi kirahisi. Ule mto anaotumia na kisha kujaribu kuvuta hisia kama vile yuko na mumewe, tayari ni pepo la ngono hujipenyeza na baada ya tendo kukamilika hutimua zake.

Na ndiyo maana baada ya hapo hujutia hali hiyo na hata pale mumewe anapokuwa naye hamfurahii kama vile akiwa na mto ule. Anachotakiwa dada huyu, kwanza ni kuuweka mbali kabisa mto ule na kisha kuchukua Biblia yake na kuisoma kama njia ya kupoteza mawazo juu ya mto wa kulalia.

Ndani ya Biblia Takatifu yapo mambo mengi sana yenye faraja. Na kila mstari ndani yake ipo sauti ya Mungu. Tukumbuke neno la Mungu lina nguvu kuu ambayo huwezi kuiona kwa macho. 
Chanzo:nipashe

Tatizo la ndugu yetu huwakumba watu wengi. Huyu katumia mto lakini wengine hutumia vitu vingine..Na shetani hujipenyeza eneo hilo la mahusiano ili kuivuruga amri ya sita ndani ya maandiko matakatifu ya Biblia kuwa Usizini. Japokuwa mtu yuko na mwezake kihalali, lakini bado ibilisi hushambulia.

Nilishuhudia mama mmoja akieleza wazi kuwa anapokuwa na mumewe humkwepa lakini awapo ndotoni yupo mtu humjia na kufurahi naye. Kumbe lijamaa hilo analoliona ndotoni ndilo linalompotezea hamu katika kumpenda mumewe.

Hili ni tatizo. Mama huyu tatizo lake limekwisha baada ya kuombewa kanisani na mambo yake ni mazuri, mahusiano na mumewe yamerejea. Ndiyo maana nikamshauri bibie hapo juu kwamba azame kwenye maombi anaweza kufunguliwa katika hicho kifungo cha ibilisi anayejulikana kama jini mahaba.

Mpenzi msomaji, hili ni tatizo katika ulimwengu wa kiroho ambalo yafaa kupambana nalo ili kulipatia jawabu. Hili liko kwa wanawake na wanaume pia. 

Tena wanaume ndiyo huwa mbaya zaidi hasa pale hata nguvu zao huwa hafifu. Hiyo siyo kawaida lipo tatizo lililojificha ambalo pengine hujitokeza katika ulimwengu wa kiroho.

Hivi umewahi kujiuliza kwanini waganga wengi wa kienyeji hutangaza dawa za kuongeza nguvu za kiume? Hii ni kwa sababu wanajua nini kinachofanyika katika ulimwengu wa kiroho ambako nako nguvu za giza zimeweka makao yake makuu.

Lakini mwenye matatizo ya aina hii, akizama kwenye maombi, Mungu aweza kumfungua kutoka kwenye vifungo hivyo vya shetani. Hebu jiulize; kwanini mahusiano na mkeo au mumeo yalikuwa mazuri na ghafla unafurahia mto na siyo mwenzio? Ipo shida hapo. Yupo adui amepenyeza kuharibu ndoa yenu. 

Lazima sasa upambane kumpiga huyo adui kwa maombi ya nguvu na bila shaka utajinasua. Kwa sababu neno la Mungu linasema kitabu cha Mathayo Mtakatifu sura ya 15 mstari wa 13 kwamba “Kila pando asilopanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa”. Hilo ni pando lazima ling’olewe kwa maombi.

No comments:

Post a Comment