MTOTO Lusia Moga (2) aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha Julai 8, mwaka huu kati Kijiji cha Bukore wilayani Bunda, Mara amekutwa akiwa mtupu nyumbani kwa Magembe Nyabu, mkazi wa kijiji hicho.
Kupatikana kwa mtoto huyo juzi alfajiri kuliibua hofu ya kuwepo kwa ushirikina iliyotawala kwa wazazi wa mtoto huyo na wakazi wengine kijijini hapo.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bukore, Moshi Madeni, alisema licha ya mtoto huyo kukutwa utupu, alikuwa amenyong’onyea kwa sababu ya njaa.
“Tulipomwona watu walijaa kumshuhudia, lakini mama yake alikataa kumbeba hivyo mtoto huyo alibebwa na mtu mwingine. Kitu cha kwanza alipewa uji kwa sababu alikuwa na njaa.
“Mpaka sasa mtoto huyo anaendelea vizuri, taarifa polisi tumepeleka na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusu tukio hilo,” alisema ofisa mtendaji.
chanzo:tanzania daima
No comments:
Post a Comment