Monday, 14 July 2014

Penny achumbiwa, amsahau Diamond

HATIMAYE aliyekuwa mpenzi wa staa wa muziki wa Bongo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ amesema amepona maumivu ya moyo baada ya kuvishwa pete ya uchumba.
Penny ambaye alionekana kuumia sana na kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari baada ya kumwagana na staa huyo, aliweka picha ya kuonyesha pete hiyo katika ukurasa wake wa instagram.
Kwa mujibu wa Penny, kidonda chake kimepona baada ya kumpata mtu ambaye atammiliki moja kwa moja.

Penny alisema baada ya kumwagwa na staa huyo, kaka zake ndio walikuwa faraja kwake kutokana na kuona kwamba ndugu yao kaumia sana.
“Kiukweli sikutegemea na wala nilikuwa sijajiandaa, ilikuwa ghafla sana, kwa sababu nilimpenda nilishindwa kujizuia, kila aliyenifahamu aliniona kama nimebadilika, sikuamini kilichotokea. Namshukuru Mungu nimesahau, kila mmoja yupo na maisha yake kwa sasa,” alisema.
chanzo:tanzania daima

No comments:

Post a Comment