Mwenyekiti wa Kitongoji cha Songambele, Kata ya Ilela Tarafa Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi, Richard Madirisha (31), ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na kutenganishwa na kiwiliwili na kisha kunyofolewa viungo vya mikono na miguu na sehemu za siri na kichwa chake na viungo hivyo kupikwa ndani ya safuria kama mboga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari mauaji hayo ya kikatili na kutisha yalitokea jana saa 5.30 usiku nyumbani kwa marehemu.
Alisema watu hao waliodaiwa kuwa na mapanga waliingia chumbani kwa marehemu na kumlazisha mkewe ajifiche kwa kujifunika na shuka usoni.
Alisema baada ya mkewe kujifunika walianza kumchinja marehemu kwa kutumia panga huku mkewe akiwa anasikia jinsi marehemu akilia kwa uchungu.
Kidavashari alisema baada ya kumchinja walichukua kichwa na kukiweka kwenye safuria na maji na kukipika kwenye moto uliokuwa unawake nje ya nyumba ya marehemu.
Alisema kisha walirudi ndani na kunyofoa sehemu za siri, mikono na miguu na kuziweka kwenye safuria jingine kwenye moto na kutokomea kusikojulikana huku viungo hivyo vikiendelea kuchemka ndani ya safuria hizo.
Kidavashari alisema mke wa marehemu baada ya kuona watu hao wametokomea alitoka nje na kwenda kutoa taarifa kwa majirani ambao walifika kwenye eneo hilo na kukuta viongo hivyo vikiwa ninaendelea kuchemke kwenye safuria hizo huku kiwailiwili chake kikiwa ndani ya chumba chake
Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauwaji kimetokana na visa vya marehemu na mtu mmoja ambae walikuwa wakiishi nae Tabora ambae alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa amemnyanya mwanamke ambae walikuwa na mahusiano nae ya kimapenzi ambae marehemu aliamua kuhama nae kijijini hapo na kuhamia nae kijiji cha Songambele Wilaya Mlele
Kamanda Kidavashari alieleza jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limewakamata na linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo ya kikatili
chanzo:nipashe
No comments:
Post a Comment