IMEELEZWA kuwa chanzo cha kuporomoka kwa elimu nchini kunatokana na serikali kushindwa kuwekeza katika sekta hiyo.
Akizungumza katika kipindi cha Tuongee Asubuhi kinachorushwa hewani na Star Tv, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu (CWT) Ezekeli Oroch alisema tangu kuanza kwa masharti ya Benki ya Dunia, elimu inashuka siku hadi siku.
Oroch alisema hayo hakuna jitihada za makusudi zinazofanywa na serikali kuhakikisha elimu inakua, “Kipindi cha utawala wa awamu wa kwanza elimu ilikuwa inathaminiwa tofauti na sasa mfano halisi ni katika kuripoti kituo cha kazi mwalimu alikuwa akilipwa posho yake pale pale.”
Akitoa mfano, Naibu Katibu Mkuu huyo alisema mwaka 2009 walimu walishindwa kupandishwa vyeo na kiasi cha sh bilioni 20 zilirudishwa hazina na kusisitiza kwamba serikali inakosa usikivu kwa wafanyakazi wake hasa walimu kwa kuwa wanapopandishwa daraja mishahara haipandi.
“Mwalimu anahamishwa lakini hawalipwi gharama za kuhamishwa ingawa jambo hilo limekuwa likisemwa na baadhi ya viongozi wakuu wa nchi lakini hakuna jitihada zinazofanywa,” alisema.
No comments:
Post a Comment