Hayawi hayawi yamekuwa ndani ya Wembley, 2011. Historia ya mashindano ya mabingwa ya Ulaya leo imeweza kugeuzwa na kuandikwa kivingine kabisa. Barcelona wameweza kuchukua ubingwa huo kwa mara mbili kwenye kipindi cha miaka mitatu, kitendo amabcho hakijawahi kufanywa na timu yeyote ya Ulaya. Ulikuwa ni mchezo wa kusismumua na hauna maelezo ya kuweza kuusimulia kama ulishidwa kuweka jicho lako kwenye luninga (TV).
Manchester United wameshindwa kufanya kilichotakiwa ambacho ni kufunga magoli na si kuzuia timu pinzani kufunga goli. Japokuwa mechi ilitawaliwa na kandanda safi kutoka kwenye timu zote mbili lakini mshindi alikuwa katoka timu kwenye timu moja ambaye ni Lione Messi. Messi aliyeiongezea matumaini yake kushinda mechi hiyo baada ya kuachia mkwaju mkali kutoka nje ya eneo la hatari kwenye lango la Manchester United na kuiandikia timu yake bao la pili.
Kwa hakika kikosi hiki cha Barcelona kinastahili ubingwa kwa mchezo na ufundi waliouonyesha uwanjani. Ila swali linabaki kwa kocha wao kijana anyechipukia kwenye hii taaluma ya kufundisha kabumbu kama atabaki na timu hii msimu ujao. Minong’ono iliyopo ni kuwa hii itakuwa mechi yake ya mwisho kwa Barcelona basi tusubiri kwa hilo. Mlango wa timu ya Chelsea bado uko wazi waungwana lakini swali ni kwanini anataka kuondoka kwenye timu kama hiyo ina kila kitu ambacho watu wengi wanafikiria kuwa navyo?
No comments:
Post a Comment