Friday, 25 May 2012

ANITA: SIJAONA MTOTO WA KUNIFUNIKA!!


MWIGIZAJI aliyejizoleaga umaarufu wakati akiwa na kundi la Kidedea, Salwa Mazurui ‘Anita’, amesema pamoja na kuibuka kwa vipaji vingi vya watoto katika tasnia ya uigizaji hadi leo hajaona mtoto aliyemfunika kwa kipaji.
Akizungumza na Tanzani Daima, Anita alisema anajiamini uigizaji wake ulikuwa wa aiana yake na ndio maana hadi leo akiwa na miaka 23 ambapo kapita umri wa mtoto, kila anapopita jina lake haliishi kuitwa.
Hivi karibuni msanii huyu alipotea katika fani ya uigizaji kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu lakini kwa sasa ameahidi kurudi kwa kasi.

chanzo: Tanzania daima

No comments:

Post a Comment