WAKATI kukiwa na habari kwamba mwanamuziki wa bongo fleva, Ally Timbulo ’Timbulo’ wimbo wake ‘Wa leo wa kesho’ aliutunga maalumu kwa ajili ya aliyekuwa x-girl friend wake, Jacline Pentezel, dada huyo ameruka kimanga madai hayo na kusema hajawahi kutembea na mwanamuziki huyo.
Dada huyo anayetisha kunako anga za filamu ambaye pia alishawahi kuchukua taji la Miss Upanga mwaka 2005, alisema kwamba hajawahi kutembea na mwanamuziki huyo na kudai kwamba habari za kuhusu mahusiano yake hayo zimekuwa za kuvumishwa tu.
Alikwenda mbali zaidi na kusema kwamba haitaji kabisa kumuongelea Timbulo katika vyombo vya habari kwa sasa kwa madai kwamba amekuwa akimuongezea ujiko kwa jambo ambalo halina ukweli wowote.
No comments:
Post a Comment