Saturday, 12 May 2012

CHILO HATAKI KUJIGHARAMIA!!!


MWIGIZAJI mwenye umri mkubwa katika tasnia ya uigizaji, Ahmed Ulotu ‘Mzee Chilo’, amesema wasanii ambao wamekuwa wakiigiza katika filamu mbalimbali hapa nchini, hawapaswi kujigharamia mavazi na badala yake gharama hiyo inatakiwa kulipwa na mwenye filamu.
Mzee huyu alibainisha kwamba, katika nchi zilizopiga hatua kwenye tasnia hii, pamoja na wasanii wake kulipwa vizuri tofauti na wa hapa kwetu, wenye filamu wamekuwa wakiwagharamia kila kitu, ikiwemo nguo.
Hata hivyo alikiri kwamba yote haya yametokana na serikali kuicha fani pembeni ambapo kama ingetumiwa vyema, ingeweza kuliingizia taifa na wao wenyewe mapato kwani wanachoambulia kwa sasa ni utani kwao ukilinganisha na kazi kubwa ambayo wamekuwa wakiifanya ya kuelimisha jamii.

No comments:

Post a Comment