Saturday, 12 May 2012

MASTAA WA KIKE WASHUKIWA!!!


MWANADADA ambaye anatisha kwa sasa kutokana na kuonekana  katika video mbalimbali za wanamuziki wa bongo fleva, Agnes Gerald ‘Masogange’, amewashukia mastaa wa kike wa bongo movies, akisema kuwa, wamekuwa wakiwadharau wasichana wanaofanya kazi kama yake.
Agnes ambaye sasa hivi anaonekana katika video mpya ya ‘Magumegume’ ya Baranaba, anasema waigizaji hao wanatakiwa kujua kuwa hata wao hiyo ni kazi yao kama zilivyo kazi nyingine na kuwataka kuacha tabia hiyo mara moja.
 “Yaani hata tukikutana nao klabu au kwenye shughuli inayokutanisha watu wengi, utawaona wanatunyali na kutuona kama takataka, jamani wajue nasi kupitia kazi hiyo tunaingiza fedha za kuendesha maisha yetu kama ilivyo wao,” alisema dada huyo

No comments:

Post a Comment