Mheshimiwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Damian Komba.
HATIMAYE siri ya madai kuwa Mheshimiwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Damian Komba na msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni wapenzi, sasa mambo hadharani, Risasi Mchanganyiko linakupa ukweli.
Mambo hayo ambayo yamekuwa katika vinywa vya watu na kuzagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwa muda mrefu, yamewekwa kweupe na Mheshimiwa Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa la Tanzania One Theatre (TOT).

LAIVU ITV
Akizungumza katika Kipindi cha Shamsham za Pwani kinachoongozwa na Mtangazaji Hawa Hassan kupitia Runinga ya ITV Jumamosi iliyopita, Kepteni Komba alifunguka kuwa hajawahi kutembea na msanii huyo kama watu wanavyodai.

HUYU HAPA KEPTENI KOMBA
“Huwa ninawasaidia wasanii wa jinsi zote lakini watu wakiona nimemsadia msanii wa kike, wanavumisha kwamba nimemtafuna,” alisema Kepteni Komba.
Alikiri kuwa alishawahi kumpa Lulu gari lake la kifahari pale msanii huyo alipokwenda na marehemu Steven Kanumba kumuomba kwa ajili ya kumpokea mgeni wao, staa wa filamu za Kinigeria, Ramsey Nouah alipotia maguu Bongo miezi kadhaa iliyopita.
“Siyo yeye peke yake, hata JB (Jacob Steven), Ray (Vincent Kigosi) na Kanumba wameshafika kuniomba hata nyumba yangu kufanyia maigizo nikawapa lakini ninapomsaidia JB hawasemi kwa kuwa ni mwanaume, ila nikimsaidia msanii wa kike, watu (wambeya) wanasema nimemtafuna,” alisema Komba kwa mshangao“Huwa ninawasaidia wasanii wa jinsi zote lakini watu wakiona nimemsadia msanii wa kike, wanavumisha kwamba nimemtafuna,” alisema Kepteni Komba.
Alikiri kuwa alishawahi kumpa Lulu gari lake la kifahari pale msanii huyo alipokwenda na marehemu Steven Kanumba kumuomba kwa ajili ya kumpokea mgeni wao, staa wa filamu za Kinigeria, Ramsey Nouah alipotia maguu Bongo miezi kadhaa iliyopita.
ENDELEA KUSOMA HAPA: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/lulu-komba-mambo-hadharani
No comments:
Post a Comment