AKIWA katika Jiji la Mumbai nchini India kwa ajili ya kumuuguza mumewe Sadiki Juma Kilowoko, staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma amelazwa katika hospitali ya Saifee kutokana na uchovu.
Akizungumza na Tollywood Newz hivi karibuni kwa njia ya simu, Wastara amesema kuwa alijisikia mchovu mara baada ya kufika nchini humo na madaktari wakalazimika kumpumzisha.
“Nilipofika tu India nilikua mdhaifu, nilipoteza network zote ikabidi nilazwe kwa sababu nilikua hoi, hapa penyewe nimelazwa lakini naendelea vizuri,” alisema.
Kuhusu maradhi yanayomsumbua mumewe Sajuki, Wastara amesema anaendelea vizuri kwa kuwa ameanza kuongea na kukaa mwenywe kwa hivi sasa.
Hata hivyo, Staa huyo amesema kuwa kabla ya mumewe kutibiwa ugonjwa uliompeleka India, amegundulika kuwa na matatizo ya pumzi, hivyo anatibiwa kwanza ugonjwa huo kabla ya kufanyiwa upasuaji.
http://www.globalpublishers.info/
No comments:
Post a Comment