MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Hamisi Yahaya (22) amekutwa amekufa chumbani kwake katika hosteli binafsi iliyopo eneo la Kijitonyama.
Polisi wamedai kuw amwanafunzi huyo amekufa kwa kujinyonga. Aidha kondakta wa daladala, Ally Saidy (24) amekufa papo hapo baada ya kuanguka kwenye mlango wa gari alipokuwa akining’inia. Matukio hayo ya vifo yalitolewa taarifa jana na makamanda wa Polisi kwa nyakati tofauti.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela alisema mwanafunzi huyo wa chuo cha Tumaini alikutwa juzi saa 4:00 usiku ndani ya chumba chake namba 203 akiwa ananing’nia kwenye kamba.
Maiti imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala. Kuhusu kifo cha kondakta, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Faustine Shilogile alisema tukio hilo ni la juzi saa 2:30 asubuhi eneo la Gongo la Mboto Mwisho wa Lami, barabara ya Pugu.
ENDELEA KUSOMA HAPA: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=30511
No comments:
Post a Comment