Thursday, 24 May 2012

MSIBA WA MAFISANGO NA KANUMBA MSHANGAO!!!!


                                                        MAFISANGO
KIFO cha kiungo mshambuliaji wa Timu ya Simba ya Dar es Salaam, Patrick Mutesa Mafisango kimetonesha kidonda cha marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ kufuatia kuibuka kwa mapya ya kushangaza.
Tayari Amani limeshapokea malalamiko kutoka kwa mashabiki wa soka Bongo kuwa mastaa wa filamu hawakuonesha ushirikiano kwenye kifo cha Mafisango kama wachezaji wa soka na michezo mingine walivyofanya kwa Kanumba.
Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili ambao hawakuwa tayari majina yao yaandikwe, walisema kuwa wakati wa kifo cha Kanumba ‘kampani’ kutoka katika michezo ilikuwa kubwa kuliko walivyofanya watu wa maigizo kwenye kifo cha Mafisango.
JINSI YA KUWALILIA
Wakati hayo yakiendelea, Amani limeelezwa kuwa kuna utofauti mkubwa wa jinsi wachezaji walivyopokea habari za kifo cha Mafisango na kuwa hata namna ya kumlilia ilikuwa tofauti na walivyofanya mastaa wa filamu kwa Kanumba.
Ikadaiwa kuwa katika msiba wa Mafisango, wanasoka wengi wa kiume hata wale ambao siyo wa Simba walishuhudiwa wakishindwa kujizuia na kuangua kilio hadharani tofauti na wasanii wa filamu wa kiume ambao hawakuonesha majonzi mazito kwenye msiba wa Kanumba.
Aidha, ilielezwa kuwa kwa Mafisango waliokuwa wanalia kupita maelezo ni wanaume tofauti na ilivyokuwa kwa marehemu Kanumba ambapo waliokuwa wakilia na kuzimia ni wanawake na ilifikia hadi hatua ya mwanamke mmoja mkoani Pwani kunywa sumu baada ya kusikia taarifa za kifo cha mwigizaji huyo.
“Ina maana kiwango cha uvumilivu baada ya kutokea kwa kifo cha mtu kwa wacheza sinema ni kikubwa kuliko kwa wacheza mpira?” alihoji mtoa habari mmoja aliyezungumza na gazeti hili.
ENDELEA KUSOMA HAPA: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/msiba-wa-mafisango-kanumba-mshangao

No comments:

Post a Comment