Monday, 21 May 2012

SHIBUDA AWAVURUGA WAKUU WA VIJANA CHADEMA

MPASUKO ndani ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) unaohusu kinyang’anyiro cha urais 2015, sasa ni dhahiri baada ya viongozi wa taifa wa chama hicho kuanza kulumbana hadharani. 

Jana Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Juliana Shonza aliitisha kikao na kuweka wazi msimamo wake kumpinga Mwenyekiti wake, John Heche, kuhusu kinyang’anyiro hicho. 

Shonza alipinga kauli ya Heche dhidi ya kada wa chama hicho na Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda kwamba hataruhusiwa kugombea urais kupitia chama hicho baada ya kuatangaza nia katika kikao cha CCM. 

No comments:

Post a Comment