Monday, 21 May 2012

MAJAMBAZI WAVAMIA,WAPORA UHASIBU ARUSHA!!!!

MAJAMBAZI zaidi ya 20 wakiwa na silaha za jadi na moto, usiku wa kuamkia jana walivamia Chuo cha Uhasibu (TIA) kilichopo Njoro nje kidogo na Jiji la Arusha na kupora vitu mbalimbali vinavyosadikiwa kuwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 19. 

Habari kutoka chuoni na kuthibitishwa na polisi mkoani Arusha, zilieleza kuwa uvamizi huo ulifanyika saa 8 usiku na majambazi hao waliingia chumba kimoja baada ya kingine na kupora vitu hivyo bila ya kudhuru mtu. 

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho, Rajabu Lingoni alisema hawakuwa na namna ya kujinusuru kwani watuhumiwa hao wa ujambazi walikuwa wengi kupindukia. 

Lingoni alisema mbali ya kuwa wengi pia walikuwa na silaha mbalimbali, ikiwamo silaha za moto na silaha za jadi zikiwamo panga, sime, mikuki na marungu makubwa na walikuwa wakisikika wakisema yeyote mwenye kupiga simu, cha moto atakiona hatua iliyowafanya wanafunzi kukubali matokeo yoyote. 

No comments:

Post a Comment