Friday, 18 May 2012

WEMA AONJA MACHUNGU YA MUME WA MTU.


SUPASTAA wa muvi za Bongo aliye pia Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu anaonekana kuanza kuonja machungu ya kuwa na uhusiano wa kimpenzi na mume wa mtu.
Madai yanasema Wema anakumbana na kadhia hiyo kwa vile anashindwa kulala naye kwa uhuru mwanaume huyo na kumfanya aumalizie usiku akiwa na midoli kitandani.
Itakumbukwa hivi karibuni, Wema aliripotiwa kufanyiwa fujo na mwanamke aliyedaiwa ni mke wa mwanaume anayetoka naye kimapenzi kwa sasa ambaye alipata taarifa za usaliti wa mumewe.
Hata hivyo, katika picha za staa huyo za hivi karibuni, anaonekana amelala kitandani akiwa amekumbatia midoli, hali inayoashiria kuwa upweke umemsonga kuliko zamani.
Picha hizo zilipigwa miezi michache tu baada ya picha nyingine alizopiga akiwa amelala na aliyekuwa mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’ enzi za utamu wa mapenzi yao.



No comments:

Post a Comment