JUMA Ali, 48, mkazi wa Mtoni Wilaya ya Temeke, jijini Dar ambaye hivi karibuni alidai kwamba mkewe aitwaye Hadija Chande 40, amemuibia nyeti zake kimiujiza, katika habari iliyoandikwa na gazeti hili yaMUME: MKE WANGU KANIIBIA NYETI sasa furaha yake imerejea kufuatia mganga mmoja wa kienjeyji kumnyooshea mambo yake.
Akizungumza na Uwazi hivi karibuni, Juma alisema nyeti zake hizo zimerejeshwa na mganga huyo baada ya kutokuwa nazo kwa muda wa miezi miwili.
“Kwa kweli nimeteseka sana ila sasa namshukuru Mungu niko freshi, nyeti zangu zimerudi baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji huko Pwani kufuatia mke wangu kugoma kuzirejesha.
“Ilifika wakati nikahisi sistahili kuendelea kuishi kwa kuwa sikuwa mwanaume niliyekamilika lakini baada ya kushauriwa kwenda kwa wataalam, sasa mambo ni shwari,” alisema Ali.
Awali, mwanaume huyo alidai kuwa, Julai 28, mwaka huu mke wake alitoweka nyumbani na baadhi ya vitu vya ndani, aliporejea akitokea kazini hakumkuta na ndipo matatizo hayo ya kupotelewa na nyeti yalipoibuka.
Sakata hilo lilifika hadi kwenye Baraza Kuu la Waislam Tanzania, Wilaya ya Temeke ili kulitafutia ufumbuzi na Hadija alipotafutwa ili kulizungumzia hakuwa tayari kutoa ushirikiano.
chanzo:http://www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment