Thursday, 4 October 2012
UDAKU NA UDAKUZZZ:AUNT HAKOMI!
AUNT hakomi! Pamoja na kupewa onyo kali na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), huku Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) likimjadili yeye na Wema Sepetu kwa kukaa utupu jukwaani, staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amegeuka sikio la kufa baada ya kurudia tukio la aina hiyo.
Tukio hilo la aibu lililopigwa chabo na shuhuda wetu lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makonde Beach uliopo mkoani Mtwara ambapo Aunt alikuwa akipiga shoo na staa wa filamu na mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, shoo hiyo ilianza mishale ya saa 6:00 usiku ambapo kabla ya Aunt kupanda kufanya kweli huku maungo nyeti yakionekana kama kawaida yake, Shilole ndiye aliyeanza kwa kugonga masongi yake na kunengua kihasarahasara japo haikuwa ishu kwa upande wake kwani alishazoeleka.
Baada ya Shilole kubinuka kwa kumwaga radhi huku akizongwa na midume stejini, ndipo akamkaribisha Aunt ambaye alianza kukata mauno mdogomdogo kabla ya kupandwa na mzuka na kujikuta akirudia yaleyale ya kukaa nusu utupu mbele ya kadamnasi iliyofurika ukumbini humo.
Kitendo cha bidada huyo kukaa nusu utupu kwa mara nyingine ndicho kilichoibuka maswali na kuwaacha watu midomo wazi wakishindwa kuamini kama ndiye huyo anayejiita bibi harusi mtarajiwa anayejipanga kufunga ndoa siku chache zijazo.
Hivi karibuni, Aunt na Wema waliibua gumzo kufuatia kukaa nusu utupu jukwaani kwenye ziara za Tamasha la Fiesta 2012 na kutokana na walivyosemwa kwa maneno makali iliaminika watakuwa wamejirekebisha lakini Aunt anaonekana kuwa sikio la kufa.
chanzo:www.globalpublishers.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment