Tuesday 6 November 2012

WAKENYA WAKAMATWA KWA KUKUTWA NA SILAA,MAITI


JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya, mkoani Mara, linawashikilia kwa kuwahoji raia wawili wa Kenya walioingia nchini na silaha na mwili wa jambazi, Nyangarya Muniko Nyangarya aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Kamanda wa Polisi Kanda ya Tarime na Rorya, Justus Kamugisha, aliliambia Tanzania Daima kuwa walioshikiliwa kwa kuhojiwa ni Stella Mogaka (32) na Luce Mogaka (20), wote wakazi wa Manispaa ya Nakuru, nchini Kenya.
Alisema watu hao walikamatiwa eneo la Tarime, walipokuwa wakipita njia za panya na mwili wa jambazi huyo kwa kificho kwa ajili ya kuufikisha nyumbani kwao kitongoji cha Mwara, Kijiji cha Nyarwana, Kata ya Kibasuka kwa mazishi.
Kamugisha alisema raia hao wanaendelea kushikiliwa ili kujua ukweli juu ya kuwa miongoni mwa kikundi cha aliyeuawa kilichoendesha vitendo vya kihalifu katika nchi za jirani za Kenya na Tanzania, baada ya kubainika walitumia jina la udanganyifu la jambazi aliyeuawa na Polisi Kenya, Nyangarya Nyangarya kuwa aliitwa Sami Mogaka walipouchukua mwili wake chumba cha maiti Manispaa ya Nakuru kuwa ni mkazi wa Kisii na kuusafirisha kuja Tanzania visivyo.
Raia hao walikamatwa walipokutwa njia za panya na mwili huo Novemba 2, mwaka huu baada ya jambazi huyo kuuawa Oktoba 25 mwaka huu na mwenzake aliyefahamika kwa jina moja la Chacha, aliyeshindwa kufahamika uraia wake.
Nyangarya na mwenzake Chacha waliuawa na polisi Kenya walipokutwa wakiendesha uvamizi katika duka la M-Pesa safari com katika Manispaa ya Nakuru nchini Kenya.
Chanzo:daima

No comments:

Post a Comment