JULAI 30, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ililifungia gazeti la MwanaHalisi kwa muda usiojulikana, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchochezi.
Kwa mujibu wa serikali, sababu nyingine ya kufungiwa kwa gazeti hilo ni pamoja na kujenga uhasama na uzushi, likiwa na nia ya kusababisha wananchi wakose imani na vyombo vya dola, hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa nchi.
Katika tamko la serikali lililotolewa na Msajili wa Magazeti, Kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (MAELEZO), Phabian Lugaikamu, katika toleo la gazeti hilo namba 302, 303 na 304 ya mwaka 2012 na mengine yaliyotangulia lilichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.
Nimelazimika kufukunyua hilo leo ili kukumbushana juu ya uonevu dhidi ya baadhi ya vyombo vya habari, hasa vile vinavyoonekana kusimama katika ukweli huku viongozi wanaotoa uchochezi wakiachwa.
Kati ya matoleo ya gazeti hilo yanayolalamikiwa na serikali kuwa yameleta uchochezi, ni lile lililokuwa na kichwa cha habari kinachosema ‘Aliyemteka Ulimboka ni huyu hapa’. Sikutegemea wala kuamini kuwa nchi inayodai kusimama katika demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, ingeweza kuchukua hatua ya kuamua kukizima chombo hicho ili kisiendelee kufukunyua yale ambayo yamekuwa yakitendwa ovyo na baadhi ya watendaji wa serikali.
Hivi kweli serikali makini imeshindwa kuyafanyia kazi yale yaliyoandikwa na gazeti hilo na badala yake haitaki kuchokonolewa ikalazimika kulifunga gazeti hilo kwa kipindi kisichojulikana?
Sitaki kuafiki wala kukubaliana na hatua hiyo ya kimabavu. Hivi sasa japo kuna taarifa nyingi mbaya na za kichochezi zinatolewa na baadhi ya viongozi wa vyama, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.
Tukijikumbusha kauli za kichochezi zilizowahi kutolewa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni ile ya wiki mbili zilizopita ambapo Naibu Katibu Mkuu Bara, Mwigulu Nchemba ametoa kauli nzito ya kwamba anayo na anamiliki mkanda wa video ya jinsi viongozi wa CHADEMA walivyokaa na kupanga mikakati ya jinsi ya kutekeleza mauaji nchini.
Kauli nyingine ni ile ya Novemba mwaka jana, wakati wa presha ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, ambapo Katibu Mkuu wa chama hicho, Willson Mukama, aliibua madai kuwa CHADEMA walikuwa wameingiza makomandoo kutoka Afghanistan, Israel na kwingineko.
Kwa akili ya kawaida tu, inatosha kuona kuwa madai yale yalikuwa ni kejeli kama sio matusi kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini, kwamba vimelala usingizi kwa sababu kama si hivyo, isingewezekana makomandoo wavuke mipaka kisha wasafirishwe hadi Igunga.
Ndiyo maana tuhuma zile zilimtokea puani Mukama na chama chake, kwani alipotakiwa athibitishe madai yake, alishindwa huku Jeshi la Polisi likisema hakuna kitu kama hicho. Hiyo ilitosha kutoa picha kuwa, baadhi ya viongozi wa chama hicho wameanza kufilisika kifikra.
Hivi kweli Mwigulu kwa nafasi aliyonayo na anavyopenda kutaka kuzidi kuwa maarufu anashindwa kuufikisha mkanda huo katika vyombo vya dola ili viongozi hao wa CHADEMA waweze kuchukuliwa hatua na hata kufunguliwa mashitaka ya mauaji?
Je, huu sio uchochezi wa moja kwa moja? Serikali inapaswa kufika mahali kuwa na washauri makini. Nasema hivyo kwa kuwa haiwezekani gazeti ambalo limekuwa ni msaada kwenu la kusema ukweli, leo mkaamua kwa makusudi kulifungia kwa vile tu mna uwezo wa kufanya hivyo.
Siku zote vurugu zinaanzishwa na baadhi ya watendaji wasio na lengo jema kwa Watanzania. Niliamini kuwa kabla ya kuamua kulifungia MwanaHalisi, kuna hatua ambayo ingeweza kufanyiwa kazi, ikiwa ni pamoja na kulifungulia mashitaka gazeti hilo kama ilivyofanya kwa gazeti hili, ambapo kesi yake ipo mahakamani kwa kuonekana kuandika makala ya kichochezi kwa vyombo vya dola.
Sitaki kugusia sana huko ili nisije nikaonekana nimeingilia uhuru wa kimahakama. Lakini tujiulize uchochezi huu wa viongozi wetu, serikali imekuwa ikiangalia kwa jicho lipi?
Pia vyombo vya dola navyo vina mkakati gani katika kudhalilishwa na baadhi ya viongozi hao? Nasema kudhalilishwa kwa kuwa haiwezekani Mwigulu akasema ana mkanda wa mauaji halafu hakuna hatua inayochukuliwa na vyombo vya dola.
Hapa ndiyo wanataka kudhihirisha kuwa kuna uhusiano wa karibu baina ya viongozi wa kiserikali, kichama na vyombo vya dola, ndiyo maana wakati yanapotolewa matamshi ya kichochezi wanagwaya kuwachukulia hatua viongozi hao wahusika.
Hata hivyo Watanzania wanaamini kuwa viongozi wa aina hiyo, wanaotoa matamko ya kichochezi wanatakiwa kupuuzwa na kuwaona kama wachumia tumbo wanaotoa kauli hizo za propaganda za kipuuzi ili kuhakikisha wanabaki katika nafasi zao.
Nikifukunyua katika MwanaHalisi, nilitegemea habari ile iliyowatia matatani baada ya kuichapisha ingekuwa ni msaada mkubwa kwa serikali kwa kuwa ingeweza kumkamata huyo aliyetajwa na kumuhoji kwa kitendo cha kuichafua Ikulu.
Nasema hivyo kwa vile hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuifananisha Ikulu kuwa ni mahali patakatifu, hivyo kitendo cha kudaiwa kuwa sehemu ya watu wanaofanya kazi huko ni wakatili sio chema hata kidogo.
Tukumbuke kuwa taifa hili ni la Watanzania wote, hakuna aliye juu ya sheria. Ni muhimu kuwa kama kuna watu wanaodaiwa na kutajwa katika matukio ya kuendesha ukatili, wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na sio serikali kukimbilia kufunga magazeti kwa vile yamekuwa yakitoa taarifa zinazoonekana kuwa na ukweli, huku viongozi wanaohatarisha amani ya taifa hili iliyodumu kwa miaka 50 wakiachwa.
Tunafahamu kuwa pasipo propaganda siasa haiwezi kunoga, lakini ni muhimu viongozi hao wakatathimini propaganda wanazozitoa kama zina tija kwa taifa au ni sehemu ya kuongeza chuki na uhasama kwa serikali iliyopo madarakani.
Nalazimika kusema hivyo kwa vile Watanzania wa leo sio wa juzi wala jana, wameamka wanajua kuchuja pumba na mchele, wanajua ni kwanini MwanaHalisi limefungiwa, ni kwa vile lilikuwa likigusa maslai ya wakubwa.
Taifa linaloimba demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, haliwezi kujengwa kwa mtindo huo. Kama kuna hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa wale wote wanaoonekana kutoa uchochezi basi zifanyike kwa usawa na sio kumpendelea fulani na mwingine kumuonea.
Kama tutaendeshwa hivyo tukubali siku moja kuona amani iliyopo ikitoweka, sitaki tufikie huko bali ni muhimu kuweka usawa katika kila jambo linalojitokeza katika taifa hili.
chanzo:daima

No comments:
Post a Comment