Tuesday, 29 January 2013

Mtoto wa Karume alipuliwa Zanzibar


MWAKILISHI wa Jimbo la Magomeni (CCM), Salmin Awadh Salmin, amesema ameshagazwa na mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Shumbana Amani Karume, kuungiwa umeme bure na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).
Alitoa tuhuma hizo wakati akichangia ripoti ya uchunguzi kuhusu ubadhirifu katika shirika hilo iliyowasilishwa na mwenyekiti Kamati ya Kuchunguza Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma, Ali Omar Shehe.
Awadh alisema kwamba kitendo cha kumuungia umeme bure mtoto huyo wa kiongozi mstaafu katika kitega uchumi chake ni kwenda kinyume na misingi ya utawala bora Zanzibar.
Alisema kwa mujibu wa ripoti ya PAC, mtoto huyo aliungiwa umeme bure na kutumika nguzo 31 kuvuta umeme kutoka umbali wa kilomita 2.5 wakati wananchi wanyonge wamekuwa wakitozwa gharama Zanzibar.
Alisema kwamba kitendo hicho lazima kipigwe vita kwa sababu kimelenga kuitafuna nchi na kuvuruga misingi ya utawala bora.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment