Saturday, 2 February 2013

Jina la Lulu latumika kutapeli ‘Facebook’


BAADA ya kurejea uraiani, msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’, baadhi ya watu wameibuka na kutumia jina lake na baadhi ya wasanii katika mtandao wa kijamii wa Facebook kujipatia fedha kwa madai msanii huyo anahitaji kusaidiwa.
Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na Clouds FM, msanii aliye karibu na familia ya Lulu, Mahsen Awadh ‘Dk. Cheni’, alisema wametaarifiwa na watu wao karibu kuwa wamesoma ujumbe wao katika Facebook kuwa wanaomba fedha kwa ajili ya Lulu kwa ajili ya kumsaidia katika kesi inayomkabili.
“Mimi sijui nchi yetu inaelekea wapi, tunashindwa kumuombea mwenzetu afikie pazuri badala yake tunatafuta njia ya kuiba kupitia matatizo ya mtu; naomba nieleweke kwamba mimi siko katika mtandao wowote na wala sijawahi kujiunga na mitandao hiyo, hivyo hao wanaotumia jina langu na la Jokate ni matapeli wakubwa na kaeni nao mbali,” alisema Dk. Cheni.
Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya aliyekuwa nguli wa filamu Tanzania, marehemu Steven Kanumba, Aprili 7 mwaka jana nyumbani kwake Sinza, Vatican, ambapo alikuwa mahabusu hadi Januari 29 mwaka huu alipopata dhamana.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment