SHINDANO la Big Brother Africa kwa msimu wa nane linatarajiwa kuanza rasmi Mei 26, ambapo mshindi anatarajiwa kuibuka na dola za Marekani 300,000, sawa na sh milioni 450.
Shindano hilo lenye mashabiki wengi vijana kwa mwaka huu litafahamika kama ‘The chase’ na linatarajiwa kuwakutanisha washiriki 28 kutoka nchi 14 barani Afrika ambapo watakaa kwa siku 90 nchini Afrrika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika mitandao mbalimbali na Mkurugenzi Mtendaji wa Mnet-Africa, Biola Alabi, alieleza kuwa wanatarajia kuwapatia mashabiki burudani kabambe kupita shindano hilo.
“Tunatarajia kuwapatia watazamaji wetu shoo kabambe na isiyosahaulika, tumejipanga kuhakikisha burudani ndani ya jumba hilo inakuwepo, kutakuwa na michezo mbalimbali ya kuburudisha, kusisimua na hata kushangaza, na ninaamini shindano la mwaka huu litashinda mashindano yote yaliyowahi kupita kutokana na ubora wake,” alisema Alabi.
Kwa upande wa Tanzania mpaka sasa hajafahamika mshiriki atakayeiwakilisha nchi licha ya baadhi ya wasanii maarufu kutajwa kuchukua fomu, wakiwamo mwanamuziki Abubakari Katwila, maarufu kama‘Q Chillah’, Hemed Suleiman, P.H.D, Khaleed Mohamed, T.I.D, muigizaji wa filamu, Wema Sepetu na Venance Mushi, aliyewahi kuwa mshindi wa pili wa shindano la Maisha Plus, 2012 na wengineo.
chanzo:daima
No comments:
Post a Comment