MABAKI ya mwili wa mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 ambaye jina lake halikufahamika, yamekutwa eneo la Magereza, Kata ya Miyomboni Kitanzini, Manispaa ya Iringa.
Walioyakuta ni maofisa wa magereza ambao walikuwa katika eneo hilo na wafungwa wakikata miti kwa ajili ya kuni.
Wakizungumza na Amani, baadhi ya mashuhuda walidai kuwa mwanamke huyo inaonekana siku ya kifo chake alikuwa amevaa suruali nyeusi, kilemba cha kitenge chenye madoa mekundu, njano, meusi na meupe pamoja na skafu ya rangi nyeupe na nyeusi.
Mashuhuda hao walidai kuwa mwanamke huyo alipoteza maisha kwa zaidi ya wiki mbili nyuma kutokana na mabaki hayo kuharibika kupita kiasi na kukauka.
Mazingira ya kifo cha mwanamke huyo yalionesha utata kwa kuwa hata polisi waliofika eneo la tukio, walikiri kutokuwepo kwa taarifa yoyote ya mtu kupotea na kwamba inawezekana alivamiwa ama alikufa kwa matatizo yake au alikuwa akitoka hospitali ambayo ipo jirani na eneo hilo.
Mabaki ya mwili huo yalichukuliwa na polisi na kuhifadhiwa katika Chumba cha Maiti cha Nina Marwaha cha Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa.
chanzo:.globalpublishers
No comments:
Post a Comment