Monday 3 March 2014

Baba wa kambo alinirubuni kimapenzi, nashindwa kumwambia mama yangu!

“Naitwa Jesi M naishi mbele kidogo ya Tegeta, DSM. Naomba ushauri maana yaliyonikuta ni makubwa. Kwanza naishi na familia yangu ila ni baba  wa kambo.
 
Muda mrefu baba yetu huyo amekuwa akinitaka kimapenzi lakini namkatalia na kwa vile nashindwa kumwambia mama, na hata  mama zangu wakubwa nikiwaambia hawaamini.
 
 Mwaka jana mwishoni mama yangu mzazi alifiwa na mjomba wake aishie Dar lakini ikabidi wasafiri wakazike Iringa. Mama aliposafiri, huku nyumbani kuna siku baba wa kambo alinituma nimpelekee kitu chumbani, huko akaanza kunichezea.
 
Kutokana na mimi nilikuwa sijakutana kimwili na mwanaume kama mwezi mzima, alipoanza kunishika shika nikalegea na kulainika nikajikuta nimefanya dhambi kubwa ya kufanya na mwanaume wa mama yangu mzazi.
 
Ikabidi nikae kimya mpaka mama aliporudi lakini nikashindwa kumwambia. Nikawa so depressed(fadhaika sana). Hakuna mtu aliyenifanya ni feel (jisikia) furaha. 
 
Baada ya majuma kadhaa tukaenda nyumbani kwa shangazi wa mama(nashindwa hata kumuita bibi kwa kilichotokea) ambapo tuliwakuta wazima wa afya.
 
Sijui kwanini ikatokea namuonea aibu mtoto wa kiume wa shangazi wa mama lakini sikuwa free (huru) kumuangalia. Kuna picha nilikuwa nazo ikabidi nimrushie huyo mkaka kupitia whatsapp maana simu ya mama yake ilikuwa imezima.
 
Kwa sababu tulikuwa agemate(rika moja) na huyo mkaka, ikawa easy(rahisi) kuzoeana baada ya kuondoka kwao. 
 
Kesho yake asubuhi nilikuwa najiandaa kwenda kwa boyfriend wangu ndio nikaanza kupata feelings(hisia) tena za Yule mtoto wa shangazi wa mama. 
 
Sikumwambia nilienda wapi lakini baada ya siku chache nilipomwambia nilihisi kama kakasirika.
 
Mimi na GP(mtoto wa shangazi wa mama), tukawa na ukaribu kupitiliza mpaka tukawa wapenzi tena maana alirudisha furaha yangu iliyopotea.
 
Baada ya miezi kadhaa, GP akajua maisha yangu yote hadi suala la baba wa kambo. Cha ajabu alizidi kunipenda hivyo yeye akakazania lazima atamshughulikia baba yangu wa kambo kwa alichonifanyia.
 
Hadi niandikapo stori hii, mimi na GP hatupo vizuri sababu namkwepa maana mimi na yeye tunapendana sana kupita kiasi lakini kwa mila zetu  hatuwezi kuoana.
 
Napata mateso kujifanya simpendi tena, vile vile naogopa chochote atakachomfanyia baba wa kambo kinaweza kuhatarisha maisha ya familia yangu yote na mimi  nawategemea hao hao wazazi kulipa ada hasa ukizingatia nasoma nje ya nchi. 
 
Naombeni ushaui wenu jamani, nifanyeje? Dah! GOD help me!”, anamalizia ujumbe wake.
 
Mpenzi msomaji wangu, bila shaka umemsikia vema binti huyu ambaye hakika yuko njia panda. Hapa amebeba mizigo miwili mikubwa; Kwanza kitendo cha yeye kujikuta anashiriki kimapenzi na mume wa mama yake (baba wa kambo). 
 
Wakati ufumbuzi bado hajaupata, anajikuta tena anaangukia katika dimbwi la mapenzi na mtoto wa shangazi ya mama yake. 
 
Ingawa anatambua fika kwamba wawili hawa kimila hawaruhusiwi kuoana, lakini je, kwanini basi akaingia kichwa kichwa kumkubalia kuwa wapenzi kupita kiasi?(Hii siyo ridhaa yake na ndio maana anajutia matukio yote hayo).
 
Msomaji wangu, tatizo nilionalo kwa binti huyu ni kwamba amekamatwa na pepo baya sana la ngono ambalo ndilo linamtesa na kumharibia maisha yake. 
 
Haiwezekani ajue fika huyu ni baba wa kambo, na amemfanyia tendo lile baya akashindwa kutangaza hadharani ili asaidie na ananusliwe hapo alipo.
 
Pia huku akijua fika kuwa yule ni mtoto wa shangazi wa mama, halafu anamwangukia kimapenzi. Hili ni pepo baya sana. Binti huyu anahitaji maombi ya nguvu ili pepo hilo limwachie aweze kuwa huru na kuaminika kwa kile akisemacho ili wale anaowaeleza wamuelewe na kumsaidia.
chanzo:nipashe 

No comments:

Post a Comment