Friday 24 May 2013

Slaa: Simchukii JK kwa dini yake,bali utendaji kazi wake

Babati. Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Willbroad Slaa amedai kuwa anachukia udhaifu wa utendaji kazi wa Rais Jakaya Kikwete,kama kiongozi mkuu wa nchi na katu hamchuki kutokana na dini yake kama watu wengine wavyopotosha.
Dk Slaa aliyasema hayo jana kwenye maeneo ya Riroda, Galapo,Mwada,Magara,Magugu,Mutuka,Sendo na Mamire,wilayani Babati,mkoani Manyara na kudai kuwa hatanyamaza kamwe kwa kuwa wananchi hawatendewi haki na matumaini yao yanaminywa na watawala.
Alisema hatamung’unya maneno wala kusita kuendelea kusema udhaifu wa Rais Kikwete hasa katika kushindwa kuchukua au kufanya uamuzi sahihi na kwa wakati sahihi kwa sababu matokeo yake yanaathiri Watanzania wote ambao yeye pamoja na chama chake wamejitolea kuwa wasemaji wao.
“Nchi hii inavunjwa,napambana na Kikwete kwa sababu ni dhaifu,” alisema na kuongeza:
“Kuna watu wanapotosha jambo hili,mimi sina chuki na Rais Kikwete kwa sababu ya dini yake”. alisema.
chanzo:mwananchi

No comments:

Post a Comment