Msanii Winfrida Masanja ‘Kajala’ amerejea upya katika fani baada ya kumalizika kwa kesi iliyokuwa ikimkabili ya tuhuma za utakatishaji fedha kwa kuibuka na filamu iitwayo 'Heart Attack'.
Taarifa kutoka kwa mmoja wa waandaaji wa filamu hiyo ambayo iko katika hatua za mwisho, imeeleza kuwa Kajala ameigiza kama msichana wa kijijini anayefanyiwa unyanyasaji na humo ameshirikiana na wasanii kadhaa nyota, wakiwamo Mohammed Fungafunga 'Jengua', Fatuma Makongoro 'Bi Mwenda' na Lumole Matovolwa 'Biggie'.
Katika filamu hiyo, Kajala amecheza kama msichana anayelelewa na wazazi wake watata, Jengua na Bi Mwenda.
chanzo:nipashe
No comments:
Post a Comment