Lusajo chini ya ulinzi
varangati la chini ya ulinzi
wanainchi wakishuhudia tukio
Ili ndilo jeneza alikuwa ameliandaa Lusajo
ujumbe alioundaa lusajo
KIJANA Lusajo Kabuje mkazi wa kitongoji cha Isanga Kijiji cha Iwindi, Wilaya ya Mbeya ameonekana na jamii kuwa ni mtu wa ajabu na amekamatwa na polisi kabla ya kutekeleza mpango wake wa kufanya mauaji ya kutisha kwa ndugu zake.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi saa 11.24 jioni eneo la klabu cha pombe, Isanga Julai 2, mwaka huu huku akiwa na visu viwili ambavyo alikusudia kufanyia unyama huo huku akiwajeruhi polisi waliofika kumkamata kabla hajatekeleza nia yake hiyo ovu.
Kabla Lusajo hajakamatwa, alifanya vurumai kubwa ambapo alimjeruhi askari mmoja mkononi, hata hivyo walifanikiwa kumdhibiti na akafungwa pingu.
“Baada ya kukamatwa nyumbani kwake kulikutwa jeneza, msalaba, katoni ya chumvi na mafuta ya kupikia ambavyo vyote mkewe alisema kuwa aliviandaa kwa ajili ya mazishi yake, hakika huyu ni mtu wa ajabu,” alisema askari mmoja aliyehusika kumkamata
Oliver Mwaluanda ambaye ni mke wa mtuhumiwa alisema: “Alipania kuniua mimi, baba yake, dada yake kutokana na wivu, ndugu zake walikuwa wakinitetea, alinunua jeneza lake kwani alisema akituua naye atajiua.”
Baba mzazi wa Lusajo, Emmanuel Kabuje alisema kuwa kijana wake hajawahi kuwa na matatizo ya akili lakini Juni 28, mwaka huu alimtishia kumuua kwa kumkatakata vipande kwa shoka na akatoa taarifa polisi Kituo cha Mbalizi.
chanzo:globalpublisher
No comments:
Post a Comment