Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ (kushoto) akiwa na baba yake Nguza Viking ‘Babu Seya’.
Chahali aliusindikiza waraka huo na maneno akimuomba Waziri Nyalandu kwa kuwa ni mmoja wa ‘memba’ wake mtandaoni aufikishe kwa Rais Kikwete kwa kuwa ulimlenga yeye moja kwa zote.
Alimwandikia Waziri Nyalandu: “Nina imani sana kwako, mheshimiwa waziri na kwa vile Rais Kikwete yupo katika swaumu, natumaini kilio hicho kitasikilizwa.”
Kukawa mchana, kukawa usiku, siku hiyo ikaisha
WAZIRI NYALANDU AKUBALI
Kesho yake, yaani Julai 22, mwaka huu, Waziri Nyalandu alimjibu Chahali kwa kumwandikia: “Chahali copy that (nimepokea), asante kaka.”
JE NYARANDU ULIFIKISHA WARAKA KWA RAIS?
Wananchi wengi mpaka sasa wanasubiria feedback kama huo waraka ulifika kwa raisi ama la?
Nyarandu tunaomba feedback...
SEHEMU YA MANENO YA KUCHOMA YA WARAKA WA PAPII KOCHA
Baada ya salamu kwa mkuu huyo wa nchi, Papii Kocha aliyekuwa nyota wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ aliandika: “Naanguka na kushika miguu yako mitukufu mheshimiwa rais.
“Nakuomba msaada (msamaha) kwako mheshimiwa rais kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu (Kisutu).
“Mhe. Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mhe. Rais.
“Naomba huruma yako mheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninayehitaji huruma yako wewe mzazi.
“Natumaini kauli yako ya mwisho ndiyo itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu.
“Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu. Mungu akubariki.
No comments:
Post a Comment